Romans 13:8-10

Kupendana Kila Mmoja Na Mwingine

8 aMsidaiwe kitu na mtu yeyote, isipokuwa kupendana, kwa maana yeye ampendaye mwenzake, ameitimiza sheria. 9 bKwa kuwa amri hizi zisemazo, “Usizini,” “Usiue,” “Usiibe,” “Usitamani,” na amri nyingine zote, zinajumlishwa katika amri hii moja: “Mpende jirani yako kama nafsi yako.” 10 cUpendo haumfanyii jirani jambo baya. Kwa hiyo upendo ndio utimilifu wa sheria.

Copyright information for SwhNEN